Hosea 6

Israeli Asiye Na Toba


1 a“Njooni, tumrudie Bwana.
Ameturarua vipande vipande
lakini atatuponya;
ametujeruhi lakini
atatufunga majeraha yetu.

2 bBaada ya siku mbili atatufufua;
katika siku ya tatu atatuinua,
ili tuweze kuishi mbele zake.

3 cTumkubali Bwana,
tukaze kumkubali yeye.
Kutokea kwake ni hakika kama vile
kuchomoza kwa jua;
atatujia kama mvua za masika,
kama vile mvua za vuli
ziinyweshavyo nchi.”


4 d“Nifanye nini nawe, Efraimu?
Nifanye nini nawe, Yuda?
Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,
kama umande wa alfajiri utowekao.

5 eKwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande
kwa kutumia manabii wangu;
nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,
hukumu zangu zinawaka
kama umeme juu yenu.

6 fKwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,
kumkubali Mungu zaidi
kuliko sadaka za kuteketezwa.

7 gWamevunja Agano kama Adamu:
huko hawakuwa waaminifu kwangu.

8 hGileadi ni mji wenye watu waovu,
umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

9 iKama wanyang’anyi wamviziavyo mtu,
ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;
wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,
wakifanya uhalifu wa aibu.

10 jNimeona jambo la kutisha
katika nyumba ya Israeli.
Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba
na Israeli amenajisika.


11 k“Pia kwa ajili yako, Yuda,
mavuno yameamriwa.

“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,
Copyright information for SwhKC